1 Kings 9:11-14

11 aMfalme Sulemani akampa Hiramu mfalme wa Tiro miji ishirini katika Galilaya, kwa sababu Hiramu alikuwa amempatia mierezi yote, misunobari na dhahabu yote aliyohitaji. 12 bLakini Hiramu alipotoka Tiro kwenda kuiona ile miji ambayo Sulemani alikuwa amempa, hakupendezwa nayo. 13 cHiramu akauliza, “Hii ni miji ya namna gani uliyonipa, ndugu yangu?”

Naye akaiita nchi ya Kabul,
Kabul maana yake isiyofaa kitu.
jina lililoko hadi leo.
14 eBasi Hiramu alikuwa amempelekea mfalme talanta 120
Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5.
za dhahabu.

Copyright information for SwhKC